Friday, November 14, 2014

KARIMA ULIYEMSIKIVU,MPONYE WETU RAIS

(1)Ewe Ndo wetu mjamali,yetu maisha kuyalinda
    Matozi yatumwaika,wetu mpendwa dhohofu
   Yeye ndiye wetu kinara,hali kutujulia
   Karima uliyemsikivu,mponye wetu Rais.
 
(2) Maradhi yalomsibu,kitandani yamemlaza
     Baridi yatuingia,hofu yatamalaki
    Yeye ndi msikivu,tena chetu kipenzi
    Karima Uliyemsikivu,Mponye wetu Rais
 
(3) Tanzania Ndiyo kwetu,Arusha nimazilka
      Ucheshi kwake ni jadi,waalahy twafurahika
      Mpe yake nafuu, Barobaro arejee
     Karima Uliyemsikivu,Mponye wetu Rais.
 
(4) hatwishi kuweweseka,kuona yu dhohofu
      Hakimezeki chetu chakula,mioyo yaumia
      Tuumwapo yeye hutufariji,wakwanza kupiga hodi
      Karima uliyemsikivu,Mponye wetu Rais.
 
(5) Jakaya Jina lake,nahodha mwelimika
      Maradhi yamemsibu,Karima umuafu
      Yeye ni wetu mpendwa,Jahazi aliongoza
     Karima uliyemsikivu,Mponye wetu Rais.
 
(6) Beti Zangu natamatisha,chini nasujudu
     Wabara na wapwani,sote Mola tumwombe
     Ahueni ampatie,Jakaya aimarike
     Karima Uliyemsikivu,Mponye Rais.
SHAIRI LIMEANDIKWA NA HEMED KIVUYO////0655 250157
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.