LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 17, 2014

JAJI MKUU AMJULIA HALI RAIS KIKWETE MAREKANI


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe
Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba
16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins
jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika
hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa
Rais Mama Salma Kikwete. Jaji Mkuu yuko Marekani kwa ziara ya kikazi
ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria
mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi
jijini Washington na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na
marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo
ya mahakama

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali
Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya
Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada
kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  Jaji
Mkuu na ujumbe wake wako  Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja
na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa
kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na
pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo
katika ili  kupata wabia  wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama Ya
Rufani Tanzania Mhe Ibrahim Juma  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa
msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman
walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Novemba 16, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyesindikiza   msafara wa Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali
jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Msajili wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara
wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda
kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Msajili wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Mhe Ignass Kitusi  ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara
wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda
kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph
Mutta ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande
Othman kwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili
Novemba 16, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa wa Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani  Dkt. Sweetbert Mkama ambaye alimsindikiza
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali
jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages