LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2014

DK.KIGWANGALA AZUNGUMZIA AMANI NCHINI



 
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Hamisi Kigwangala akizungumza na vikundi mbalimbali mbalimbali vya Joging vilivyoshiriki katika tamasha la Mbio za Amani lililoshirikisha wawakilishi kutoka pande mbalimbali za nchi na kupokelewa na mbunge huyo ambye alikuwa mgeni rasmi, Dr. Khamis Kigwangala amewaasa wanasiasa kutoleta siasa za uchochezi hasa katika mchakato mzima wa Katiba mpya ambapo amesema waachwe wananchi wenyewe waisome waielewe na wao wataamua kama wataipigia kura ya Ndiyo au Hapana, mapokezi hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2 
Mdau wa michezo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Kanali Mstaafu Iddi Kipingu akizungumza na vikundi hivyo. 10 11 
Bw. Dioniz Malinzi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT akizungumza jambo na vikundi hivyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Tamasha la Mbio za Amani. 13 
Vikundi hivyo vikifanya mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja. 14 
Vikundi hivyo vikiimba wimbo wa Taifa.
.......................................................................
Wanasiasa wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Tanzania, ili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikisababishwa na makundi ya wanasiasa, kwa kutoa ujumbe kwa wananchi unao chochea kuvurugukika kwa amani ya Tanzania.
Akizungumza na wanamichezo wa vilabu mbalimbali vya kukimbia (Jogging) kutoka Tanzania bara na Zanzibar, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, mbunge wa jimbo la Nzega, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Tawala za mikoa na seikali za mitaa, Dk. Hamis Kigwangala, amesema wakati bunge maalum la Katiba lilipokuwa likitunga katiba inayopendekezwa, kuliibuka baadhi ya wanasiasa, waliokana kushiriki katika bunge hilo na kutofautiana katika baadhi ya mambo kuingizwa katika katiba hiyo, huku wale waliobaki ndani ya bunge maalumu la katiba kwa asilimia takriban 85 wakiheshimu maamuzi ya watanzania na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.
Hivyo amewataka wanasiasa pamoja na kuwa mapendekezo yao hayakuingia ndani ya katiba wasiwe chanzo cha kutokuridhika kwao kulazimisha na watanzania wengine wasiridhike na kwamba watanzania waachwe siku ya kuipigia kura katiba inayopendezwa itakapo tangazwa, watanzania waipigie kura ya ndio au hapana na kwamba waamue kwa utashi wao bila uchochezi wa wanasiasa.
Katika Tamasha hilo lililopewa jina la Mbio za amani 2014, Dk, Kigwangala pia amehimiza umuhimu wa kufanya michezo kila wakati, kwani michezo ni Afya, Furaha, Amani, Upendo na Ajira, huku akivitunuku vyeti baadhi ya vilabu vya Jogging kwa kushiriki katika tamasha hilo.
Tamasha hilo limeshirikisha wanamichezo wa vilabu vya Jogging kutoka Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo limeandaliwa na Faita Jogging & Sports Club ya jijini Dar es Salaam, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kuandaliwa.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages