LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 16, 2014

DK. BILAL AWATAKA VIONGOZI NA WANACHAMA CCM KUIMARISHA CHAMA KWA KUEPUSHA MISUNGUANO NA MIFARAKANO NDANI YA CHAMA

NA BASHIR NKOROMO
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal ametoa mwito kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kuacha misuguano na mifarakano ili kukiepusha  mipasuko isiyo ya lazima.

Dk. Bilal (pichani), ambaye pia ni mlezi wa Chama mkoa wa Dar es Salaam, alitoa mwito  huo wakati akiwahutubia katika mkutano uliowakutananisha viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa kujadili uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Alisema CCM ni chama pekee hapa nchini ambacho kinafanya shughuli zake kidemokrasia na ndio maana kinaendelea kushika dola na kukubalika na wananchi.

Dk.Bilal alisema  katika kipindi hiki cha mchakato wa kuwapata viongozi kuelekea katika chaguzi mbalimbali kunakuwa na changamoto za hapa na pale hivyo wenye dhamana ya kuwateua wagombea wanapaswa kutenda haki kwa kumteua yule aliyepigiwa kura kwa wingi badala ya kufanya ndivyo sivyo.

"Chama Cha  Mapinduzi ndio chama chenye dira na sera zinazotambulika hivyo viongozi wake wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha hakuna makundi yanayoweza kuwagawa wanachama" alisema Bilal

Alisema  viongozi wa chama hicho  wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote kwani uwezo wa kufanya hivyo upo kwa kuwa chama hicho kimejipanga vizuri kuanzia ngazi ya shina na kina maadili.


Bilal aliongeza kuwa kila uchaguzi unapofanyika watu na vyama vingine wanaangalia CCM imemsimamisha nani hivyo ni vizuri wakati wa uteuzi wa viongozi wanapaswa kuwa makini kwa kumchagua aliyebora.


Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema wamejifunza mengi katika chaguzi zilizopita ambapo walipoteza maeneo kadhaa kwa kuchuliwa na vyama v, kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kupata mgingine kutokana na makosa hayo.

Alisema hivi sasa mwanachama yeyote atakaye shinda kura za maoni ndiye atakayekuwa mgombea katika eneo husika labda tu awe amepita kwa rushwa na mambo mengine ambayo yatathibishwa.

Madabida alisema kwamba katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi za serikali za mitaa kulikuwa na changamoto za hapa na pale ambazo watahakikisha zinafanyiwa kazi ili mambo yaende sawa.
Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiingia ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya mkutano. (Imeandaliwa na www. habari za jamii.com)

viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa wakimkaribisha mgeni rasmi wa mkutano huo, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Garib Bilal (hayupo pichani)
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba "Gadafi" akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk. Bilal.
Makamu wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal (katikati), akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo, kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.

Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonah Kaluwa (katikati), akifurahia jambo na viongozi wenzake katika mkutano huo.

Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wanaccm wakiwa wamefurika ukumbi wa Karimjee 
katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Wanaccm wakiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages