Monday, October 6, 2014

MJUE IRENE LA VEDA, MSHIRIKI WA BBA KUTOKA TANZANIAIrene Neema Vedastous 'La Veda', Mshiriki wa Big Brother Hotshots kutoka Tanzania.
IRENE NEEMA VEDASTOUS ni msichana mrembo wa Kitanzania, mwenye umri wa miaka 23 anayeiwakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’ nchini Afrika Kusini.

La Veda katika pozi na baadhi ya mastaa.
Mrembo huyu ambaye ameshawahi kuingia 10 bora ya shindano la Miss Tanzania mwaka 2012, baada ya kutwaa taji la Miss Lindi 2012, anaingia rasmi leo tarehe 5 Oktoba 2014 kwenye shindano hilo lenye mashabiki
wengi duniani ambalo kuanzia saa 1 jioni litakua likirushwa live kupitia DSTV kwenye channel no. 198.
Irene Neema Vedastous aka Irene La Veda ni nani?
Irene La Veda, sio mrembo mpya kwenye jamii ya Watanzania kama wengi wanavyodhani, ni mrembo anayependa kujichanganya na watu mbalimbali. Hii hali imemuwezesha kufanya vitu mbalimbali na
vikubwa kwenye fani mbalimbali kama filamu, muziki, urembo, mitindo, nk.

FILAMU (BONGO MOVIES): Amecheza filamu mbalimbali ambazo nyingine zipo sokoni na nyingine bado hazijaingia mfano; KITENDAWILI, aliyofanya na msanii Rich Rich tayari ipo sokoni, LOVE IN A MESS
aliyocheza na Msungu. Mrembo huyo, pia amecheza filamu na magwiji kama King Majuto, Mzee Magali, Hashimu Kambi na Mzee Chilo ambapo filamu hizo walizocheza zitaingia sokoni hivi karibuni na zote
La Veda amecheza kama mhusika mkuu ‘Main Character’.

La Veda akiwa kazini.
MUZIKI: Kwa upande wa muziki, La Veda ni mkali sana wa kucheza na tarumbeta. Hii ni nadra sana kukutana na mwanamuziki ambaye anauwezo wa kupiga kifaa japo kimoja cha muziki.
Mrembo La Veda sio tu mkali wa kupuliza tarumbeta bali ameshatoa vibao mbalimbali kama UTANIMISS, SIMPLE LOVE, LET IT GO, na kibao kikali kinachotamba kwenye mitandao mbalimbali, kibao
ambacho kinaitangaza Tanzania katika sekta ya utalii kiitwacho TWENDE TUKATALII , Video ya wimbo huu inapatikana You tube.
Video ya wimbo wa La Veda, Twende Tukatalii.
UCHEZAJI DANSI: Mshiriki huyo ni dansa mzuri na umahiri wake tayari ameuonyesha katika video zake alizofanya pamoja na kazi nyingine za muziki alizofanya hapa Tanzania na nje ya nchi zikiwemo Uswiss na Ufaransa.
MITINDO NA UREMBO: Licha ya kuwa Miss Lindi 2012, La Veda ni mwanamitindo ambaye tayari ameshafanya 'events' mbalimbali za mitindo mojawapo ikienda kwa jina LA VEDA SHOW.
Irene La Veda ambaye hasiti kusema 'Role Model' wake ni Mama yake Mzazi, moja ya mipango yake ni kuona anafika mbali kisanaa, hivyo aliamua kwenda kukaa darasani kwenye Chuo Cha Sanaa
Bagamoyo mwaka 2012 kuongeza ujuzi na utaalamu katika fani hiyo.

La Veda (wa kwanza kulia) akiwa na baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania 2012.
Mama Mzazi wa La Veda, Mecky Sebastian anasemaje kuhusu mwanaye kushiriki Big Brother Hotshots? msikie hapa;
"Naomba akina mama wenzangu, wasanii na Watanzania wote kwa ujumla mnisaidie katika kumuunga mkono La Veda ili aweze kuiletea heshima nchi yetu na yeyote popote alipo mwenye kuitakia mema
Tanzania na Afrika Mashariki tumpe ‘support’ ya kutosha ili aweze kuibuka mshindi. Nawatakia Watanzania kila la kheri kwenye shughuli zao za maendeleo", alisema Mama Mzazi wa La Veda, Mecky
Sebastian.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.