Friday, October 10, 2014

KINANA AWATAKA VIONGOZI WA CCM MUFINDI KUSIMAMIA HAKI ZA WANANCHI WAO Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi wa Mafinga wakati akiwasili kwenye uwanja wa Mashujaa .
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana na Bi.Mwigavillo Ngole ambaye amesafiri mwendo mrefu kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
 Wazee wa Kimila wakiwa uwanjani kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo walimpa Uchifu na kumtambua kwa jina la  Galiendela Matuga .
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Johanes Kaguo akifungua mkutano na kuhutubia wananchi wa Mafinga ambapo alielezea kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa Mafinga kwa Katibu Mkuu wa CCM.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mafinga na kuwaambia kuwa Mafinga hamna upinzani ila kuna manung'ung'uniko ya wananchi ambao hawapati taarifa za kina kuhusu masula yanayohusu ugawaji na upatikanaji wa vibali vya mbao.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akihutubia wananchi wa Mafinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa
 Umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Mashujaa Mafinga kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mafinga wilaya ya Mufindi ambapo aliwaambia viongozi kuwa mstari wa mbele kusimamia haki na wajiepushe kuingia kwenye mambo ambayo yatasababisha kushindwa kuwatetea wananchi wao.
 Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamoud Mgimwa akihutubia wananchi wa Mafinga kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo alisema waombaji wa vibali ni wengi kuliko uwezo wa serikali hivyo umeanzishwa utaratibu wa kila aliyepata kibali asiombe mara ya pili.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa mbali mbali zinazohusu wilaya ya Mufindi
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi hao ambapo aliwatajia vijiji vitakavyopata umeme ,maji na umuhimu wa kujiandikisha kwenye mfuko wa afya ya jamii.
 Wananchi wakifuatilia mkutano
 Kila mtu alikaa alipoweza kumuona Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana.
 Watu walikuwa mpaka kwenye ukuta wa uwanja wa Mashujaa kumsikiliza Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Bi.Leah Msese ,zaidi ya watu 400 wamejiunga na CCM Mafinga.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Bi. Christiana Kiando wa kijiji cha Sao Hill baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.