LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 1, 2014

KINANA ATEREMKA MILIMA YA USAMBARA KWA BAISKELI AFANYA ZIARA MKINGA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi, waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiendesha baiskeli kwenda Kata ya Mg'aro katika mteremko wa milima ya Usambara, akitokea Lushoto kwenda Wilaya ya Mkinga,  mkoani Tanga jana kuendelea na ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kutafutia ufumbuzi.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiongoza msafara wa waendesha baiskeli kushuka kwenye vilima vya Usambara ambapo alijionea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwani barabara imeimarishwa na inapitika vizuri.



















 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mkinga kwenye ukumbi wa World Vision Manza.
Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima kwa lengo la kujenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza masuala ya Umoja na mshikamano wakati wa Kikao cha  wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mkinga kwenye ukumbi wa World Vision Manza.
Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima kwa lengo la kujenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.

 Bango la Mapokezi kwenye viwanja vya mikutano Duga Maforoni
 Wakazi wa kata ya Duga wilaya ya Mkinga wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

 Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe.Mboni Mgaza akijibu swali la wananchi ambao hawakulipwa pesa zao za fidia za kuvunja nyumba zao wakati wa ujenzi wa barabara.
 Lemameo Keiya akiuliza swali kujua hatama yao kwani eneo lao walilokuwa wanamiliki tangia mwaka 1940 TANAPA wamewapokonya na  kusababisha kukosa mahala pa kulisha mifugo.
 Hii ndio sare waliotupia wakina mama wa CCM Mkinga leo jioni kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages