LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 14, 2014

KINANA ASONONEWA MIKOROSHO ILIVYOKAUSHWA MKURANGA NA UGONJWA USIOJULIKANA, ATAKA WAKULIMA WAFIDIWE WASIFE NJAA

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akionyeshwa mikorosho iliyokauka katika mashamba ya wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Magawa katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, alipokagua adhari za mikorosho hiyo Sepetemba 14, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama  na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa huo. Baada ya kushuhudia madhara hayo Kinana amesononeshwa na kuahidi kulifikisha tatizo hilo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili serikali itazame njia ya kuwafidia wakulima ili kunusuru hali za maisha yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua mikorosho iliyokauka katika mashamba ya wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Magawa katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, alipokagua adhari za mikorosho hiyo Sepetemba 14, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama  na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa huo. Baada ya kushuhudia madhara hayo Kinana amesononeshwa na kuahidi kulifikisha tatizo hilo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili serikali itazame njia ya kuwafidia wakulima ili kunusuru hali za maisha yao.
 Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili katika wilaya ya Rufiji, Septemba 14, 2014, wakati akiendelea na ziara yake katika mkoa wa Pwani. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ameambatana naye katika ziara hiyo.
 Kinana akimsalimia Mbunge wa rufiji alipowasilikatika wilaya hiyo
 Kinana akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurudin Babu alipowasili katika wilaya hiyo, leo Septemba 14, 2014.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurudin Babu alipowasilina Kinana katika wilaya hiyo.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Rufiji wakiwakwenye kikao chao na Kinana, wilayani humo leo, Septemba 14, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Rufiji, leo Septemba 14,2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, akifungua Ofisi ya mafundi seremala Mbuyuni wilayani Rufiji, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama  na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa huo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia Wananchi katika mkutano wa Kinana uliofanyika katika mji mdogo wa Utete, wilayani Rufiji, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama  na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa huo.Nape amewataka wananchi kuendelea kuwa na Imani na CCM akisema ndicho chama chenye uwezo wa kutatua kero zao na ndicho chenye uhakika wa kuwa nao kwa muda mrefu kwa sababu kinaendelea kuimarika wakati vile vya upinzani vikizidi kufa.
  Katibu Mkuu wa NEC, Kinana akihutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Utete, wilayani Rufiji, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama  na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika mkoa huo.Kinana amesema, CCM itaendelea kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua katika njia iliyo sahihi.
Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, katika mkutanowa hadhara uliofanyika leo, Septemba 14, 2014 katika mji mdogo wa Utete, wilayani Rufiji mkoa wa Pwani. Jumla ya wanachama wapya 180 walipewa kadi. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages