LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 22, 2014

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO


 Magari yakivuka juu ya daraja la muda la Mto Kilombero lililojengwa kurahisisha kazi za ujenzi wa daraja la kudumu katika wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro, wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa darajan hilo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti 20, 2014.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni  Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa  Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw. Patrick Mfugale juu ya ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  Agosti 20, 2014. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe, Magufuri akifuatiwa na Mama Salma Kikwete.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu madawati mapya ya shule  ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani wa Morogoro Agosti 20, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete  na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Epauko wilayani Mahenge baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa madawati 500 na Kampuni ya Kibaran Resources Ltd inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya Graphite na Nickel mkoani Morogoro Agosti 20, 2014.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages