LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 28, 2014

UCHAGUZI DMV, CHAGUA SALMA MOSHA MGOMBEA WA UMAKAMU WA RAIS.

Wana DMV mimi ndiye kiongozi wenu imara nisiyeyumba. Nitakuwa pamoja nanyi wakati wote kwenye shida na raha kwenye dhorubana shwari kwenye matatizo na mafanikio SITAJITOA na kuwaacha njia panda kama alivyofanya mgombea mwenzangu kwenye kikao ubalozini mbele ya Tume Board, Mh Balozi  na Wagombea July 18.

Alinyoosha kidole na akasema anajiuzuru, hatogombea tena. Viongozi aina hii ndio walioifikisha Jumuia pabaya, mguu ndani mguu nje ni kigeugeu. Hapa si mahala pa kujaribu  mimi nitakuwa nanyi katika kipindi chote mtakachonipa dhamana.

Kwa heshima na taadhima naomba kura zenu mimi SALIMA MOSHI mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais.

    ZIFUATAZO NI SERA ZA ZANGU
 UZOOEFU: Nina uzoefu wa kutosha  katika maswala ya uongozi  na maswala ya mawasiliano  nimekuwa kiongozi wa muda mrefu katika upande wa sanaa na eneo langu ambalo nilikuwa naishi nimeweza kukuza na kuinua vipaji na wasanii mbalimbali ambao ni maarufu.

Aidha kwa kudhihirisha kuwa ni kiongozi mtendaji na kuonyesha mfano niliweza kushiriki katika sanaa ya nyoka na kuliletea Taifa la Tanzania, sifa pia vijana kupata ajira na kipato  na ni mzoefu katika mawasiliano kwa rika zote, wakubwa, wadogo, vijana, wazee, wageni viongozi wa serikali kwa heshima na adabu kwa kuwaunganisha wote na kuleta umoja katika Jamiiyetu.

Nikiwa hapa DMV mimi na familia yangu tumekuwa tukisaidia wanajumuia kupata ajira na tumeshasaidia zaidi ya wana-Jumuia 25 ili kuweza kujikimu na kuhamasisha kudumisha umoja katika jamii yetu                                                                                                      

 UMOJA: Nitaimarisha 'network' ndani ya Jumuia yetu ili kuwa pamoja na kuvunja makundi na kuwa karibu na Jumuia zote zilizopo DMV na STATE nyingine na kote DUNIANI.

ELIMU: Nitaishawishi serikali kupanua wigo wa kutoa mikopo ya Elimu ya juu hata kwa walio nje ili wana DMV waweze kufaidika na mikopo hiyo ya Elimu ya juu.

KISWAHILI: Nitahakikisha tumepanga mipango madhubuti kuhusu darasa la kiswahili hasa kuhusu eneo la Darasa na Walimu  na kuliendeleza hadi kwa vijana  na kuwezesha kufungua darasa hata kwa watu wa hapa wanaotaka kujifunza kiswahili kwa kulipia ili jumuia kujipatia kipato.

Pia tutawafundisha watoto wetu wajue mila na desturi zetu, Kwa kutumia taaluma yangu ya sanaa nitaanzisha kikundi cha sanaa kwa watoto na vijana ili waweze kujua Utamaduni wetu wa kucheza ngoma sarakasi maigizo n.k. hapa DMV tuna vijana wanaweza kuimba kwaya na muziki wa dansi, tutaviendeleza vipaji vyao.

AFYA: Nitasimamia upatikanaji wa BIMA Nafuu ya Afya kwa wana Jumuia kuwasiliana na mashirika mbalimbali ya Afya ili wana-Jumuia kuwe na utaratibu wa kuchekiwa afya zao kila mwaka na kusaidia Wanajumuia kuwaelekeza maeneo kwa ajili ya huduma nafuu au ya bila malipo.

AJIRA: Nitahakikisha nimesimamia Jumuia yetu kuwa na miradi ya kuingizia kipato, pia itasaidia wana Jumuia kupata ajira kama 7-11 kwa wenzetu.

MAKAZI: Nitahakikisha nimesimamia Jumuia kuweza kununua nyumba kama mradi na wakati huohuo wanaJumuia kupata sehemu ya kuishi na kulipia katika Jumuia.

DMV COMMUNITY CENTER: Nitahakikisha tumefungua Community Center yetu ili iwe sehemu ya kubadilishana mawazona kupata vyakula vya Nyumbani.

MWANASHERIA: Nitasimamia upatikanaji wa mwanasheria wa Jumuia ili awe tayari kusaidia wana Jumuia katika maswala ya sheria.

WAZEE: Jumuia inahitaji Busara za wazee, nitahakikisha tumewashirikisha wazeena kukutana nao mara mbili kwa mwaka na ili kuwaenzi.

ARIDHI: Nitaishawishi Serikali kupitia wizara yake ya Aridhi kutupatia Eneo la Aridhi na kujenga kwa pamoja Nyumba za makazi kwa gharama nafuu kinakuwa kijiji cha wana DMV hiyo imewezekana kuna kijiji cha Wasanii mkuranga.

MIKOPO: Nitazungumza na Bank mbalimbali Nyumbani ili wanaJumuia waweze kukopeshwa mikopo ya Nyumba au Biashara kwa marejesho nafuu.

MAZISHI: Nitaishawishi serikali kuweza kuchangia gharama za Mazishi pale mwanaJumuia anapofariki kwa kutoa ubani wake kwani mwana JUmuia anachangia kiasi kikubwa maendeleo nyumbani pia nitaongea na NSSF kuweza kukubali kupokea michango nusu nusu kwa dhamana ya JUMUIA na kupunguza kiasi kwa kuwa italipwa kama kikundi.

URAIA PACHA: Nitasimamia na kushawishi serikali kupitisha uraia pacha ili mMtanzania aweze kuwekeza nyumbani bila kuonekana kama mgeni ndani ya nchi yake, Nitashirikiana na viongozi wote watakaochaguliwa ili tuweze kuleta maendeleo katika jumuia yetu

 Ndugu wana Jumuia wenzangu mtakumbuka tulikuwa na kikao kwa MH Balozi JULY18 na kuhudhuriwa na Board Tume na Wagombea Mgombea mwenzangu alitamka anajitoa na hataki kugombea tena huyu ni Nahodha kweli anabahatisha wakati wowote anaweza kuacha hataweza kuwavusha mifano tumeiona hatufanyi makosa tena mimi nitakua pamoja muda wote kwa hali yote kwa heshima naomba kura zenu ahasanteni.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages