LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 24, 2014

MZEE CLEOPA MSUYA ANG'ATUKA RASMI KATIKA UONGOZI WA UMMA

Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza na kuzungumza na Waziri mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya aliyetangaza rasmi kung’atuka nafasi zote za uongozi baada ya kuitumikia serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa zaidi ya miaka 33. Mzee Msuya alitangaza hayo katika hafla maalumu iliyofanyika katika Ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Mwanga, jana.
 Mzee Msuya akiteta jambo na Rais Kikwete wakati wa hafla hiyo.
 Mzee Msuya akizungumza na kutangaza kung'atuka rasmi shughuli za uongozi katika Chama na serikali, wakati wa hafla hiyo
 Wazee wa wilaya ya Mwanga wakimkabidhi Mzee Cleopa David Msuya zawadi mbalimbali na kumkaribisha kijijini wakati wa hafla ya kumuaga kama kiongozi iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM Wilayani Mwanga jana
 Mzee Msuya akifurahia jambo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu mstaafu  Mzee Cleopa David Msuya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM mjini Mwanga,Mkoani Kilimanjaro jana  ambapo Mzee Msuya alitangaza kung’atuka rasmi kutoka nafasi zake zote za uongozi wa umma.Wengine katika picha walioketi mbele kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa KilimanjaroBwana Leonidas Gama,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, na kulia ni Wziri wa maji mbaue pia ni mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe.Picha zote na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages