BREAKING NEWS

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 11, 2014

CCM YATEUA MGOMBEA WAKE UCHGAUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA, NI GODFREY WILLIAM MGIMWA

Kamati Kuu ya CCM, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imempitisha Godfrey William Mgimwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.
   Akizungumza na waandfishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katribu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Kamati Kuu ya CCM  imemridhia Godfrey kupeperusha bendera ya CCM baada ya kukidhi vigezo licha ya kuongoza katika kura za maoni jimboni humo
   Godfrey ni Mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga na pia Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa ambaye ameliacha wazi jimbo hilo baada  kufariki dunia Januari 1, 2014.
   Pichani, Nape akimtambulisha Godfrey kwa waandishi wa habari, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Maelezo na Picha na Bashir Nkoromo wa CCM Blog
   

No comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages