Friday, July 5, 2013

MWANAFUNZI WA VETA MWENYE MAHITAJI MAALUMU AWA KIVUTIO KATIKA BANDA LA VETA.‏

  Range Jackson ambaye  ni mwanafunzi mwenye mahitaji maaalum(Matatizo ya akili katika kujifunza) walimu  wa VETA wanakataa kuwaita jina hilo kwa kuwaonyesha kuwa wanafundishika ,Pichani akiwaonyesha  askari Polisi waliotembelea katika banda lake kifaa maalumu kinachotumika kumsaidia kumfunza.Kutokana na tatizo lake walimu wa VETA wamelazaimika kumfundisha mtoto na baba yake mzazi Jackson Range ili kumrahishia mafunzo yake kwa sababu baba atakuwa anamkumbushia masomo yake aikiwa nyumbani  kwa sababu mtoto huiga mambo mazuri kutoka kwa wazazi .Katikati ni mwalimu wao Kintu Kilanga.Wananchi mnakaribishwa katika banda la Mafunzo ya Ufundi stadi VETA, mjionee mafunzo mbalimbali yanayotolewa na chuo hicho kwa vijana wetu.
Mbunge wa viti maalum  Magret Mkanga akikabidhiwa  jiko na Range Jackson ambaye ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu  wakati alipotembelea katika banda la VETA, Katikati ni mwalimu wake  Kintu Kilanga akishuhudia, Mafunzo ya Rangae yanakwenda sambamba na baba yake hayupo pichani.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.