SEKRETARIETI MPYA KUSUKUMA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM

Monday, November 19, 2012

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati  wa mkutano na waandishi wa habari leo tarehe 19 Nov.2012

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi amezungumzia ziara ya kwanza ya Katibu Mkuu wa Chama itakayoanza  tarehe 21 na kukamilika tarehe 24,Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo Lumumba, Katibu wa NEC alianza kwa kutoa shukrani kwa vyombo vya habari kwa namna vimeripoti mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi uliomalizika hivi karibuni.
 Pili ,Katibu wa NEC alizungumzia pia ziara ya siku nne katika maeneo mbalimbali ikiwa moja ya harakati za kusukuma ilani ya uchaguzi ya CCM, Katibu mkuu ,Abdulrahamu Kinana ataongozana na viongozi wengine wa Sekretarieti pamoja na Mawaziri husika katika maeneo hayo.

Ziara hiyo itakayoanza tarehe 21 mkoani Mtwara ambapo masuala mbalimbali yanayohusu wakulima wa Korosho, Bandari na miundo mbinu mingine itafanyiwa kazi, tarehe 22 Katibu atakuwepo mkoa wa Rukwa ,Sumbawanga kuangalia maendeleo ya miradi  barabara, tarehe 23 Geita, Migodi na masuala ya wachimbaji wadogowadogo,na kumalizia Arusha tarehe 24,ambapo kuna viwanda vingi ambavyo vipo chini ya wawekezaji lakini havifanyi kazi, na kusababisha tatizo la ajira na uchumi kudorora.

0 comments:

Post a Comment

Mdau, huu ni uwanja wako, uwe au usiwe mwana-CCM. Kumbuka, kwa kuwa CCM ndicho chama tawala, Maoni yako yatasaidia sana kujua wewe Mwananchi unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Toa Maoni bila hofu. Kumbuka hatutachapisha maoni yasiyozingatia utu au yenye lengo la kuchafua hali ya hewa kisiasa, kidini, kikabila, kijinsia au kuchochea mtafaruku wowote katika jamii. Usipoweza kutuma maoni yako hapa Tutumie katika email, nkoromo@gmail.com au thamani80@gmail.com au tupigie simu +255 (0) 712 498008. Mtayarishaji Mkuu, CCM Blog